14 Julai 2026 - 10:06
Kituo cha Imam Sajjad (as) Kigoma kinaendelea kuelimisha vijana na kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (as)

Chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mkuu, Sheikh Hussein Moshi Abdallah, Kituo cha Imam Sajjad (as) kilichopo Kasuko, mkoani Kigoma, kinaendelea kutoa elimu ya dini kwa vijana na kuinua bendera ya Ahlul-Bayt (as) nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Kituo cha Imam Sajjad (as) kilichopo katika kijiji cha Kasuko, mkoani Kigoma, Tanzania, kinaendelea kutekeleza jukumu lake la kutoa elimu ya dini kwa vijana na kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (as) kwa jamii.

Shughuli za kielimu na malezi ya Kiislamu katika kituo hicho zinafanyika chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mkuu wa kituo, Sheikh Hussein Moshi Abdallah, ambaye anaongoza juhudi za kukuza elimu ya dini, maadili mema na mapenzi kwa Ahlul-Bayt (as) miongoni mwa kizazi cha vijana.

Viongozi wa kituo hicho wameeleza kuwa dhamira yao ni kuendelea kuinua bendera ya Ahlul-Bayt (as) kupitia elimu, malezi na huduma za kidini, ili kujenga jamii yenye maarifa, uchamungu na mshikamano.

Kituo cha Imam Sajjad (as) pia kimetoa mwaliko kwa Waislamu na wapenda elimu ya dini kutembelea Kasuko, Kigoma, na kushuhudia kwa karibu shughuli zake za kielimu na da'wah zinazolenga kueneza nuru ya Ahlul-Bayt (as) nchini Tanzania.

Kituo cha Imam Sajjad (as) Kigoma kinaendelea kuelimisha vijana na kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (as)

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha